Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AU yataka Dk Tulia azidi kuungwa mkono uspika wa dunia

Tulia Ackson Dp AU yataka Dk Tulia azidi kuungwa mkono uspika wa dunia

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Afrika (AU) wameridhia kwa kauli moja jina la Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kuwa mgombea wao katika Umoja wa mabunge ya Duniani (Inter-Parliamentar Union -IPU).

Uamuzi wa kupitisha jina la Dk Tulia ulifikiwa kwenye mkutano wa viongozi hao uliofanyika Julai 13 na 24, 2023 walipokutana jijini Nairobi nchini Kenya.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 19, 2023 na Ofisi ya Bunge kitengo cha mawasiliano imetaja kuwa, uamuzi wa kupitisha jina la Dk Tulia ulitokana na ombi la Tanzania la kuungwa mkono kwenye mkutano huo

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi sasa Dk Tulia Ackson ameshaungwa mkono na Bunge la Afrika (PAP), Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Jukwaa la mabunge ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC-FP) ili kugombea nafasi hiyo.

Uchaguzi wa Rais wa IPU unatarajia kufanyika Oktoba 27, 2023 nchini Angola ambako Afrika itaingia na jina la Dk Tulia Akson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live