Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ADA TADEA WAZINDUA KAMPENI ZAO

Ada ADA TADEA WAZINDUA KAMPENI ZAO

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Chama cha Ada ya Tadea wamewahidi wananchi kuwaletea maendeleo makubwa nchini hususani sekta ya kilimo,afya na fursa za ajira kwa vijana na kuwataka kuendeleza amani na utulivu wa nchi yao.

Hayo ameyasema Mgombea wa Nafasi ya Urais Zanzibar kupitia chama cha Ada ya Tadea Juma Ali Khatibu wakati alipokuwa akizindua Kampeni ya chama hicho katika Kiwanja cha Magae Songea .

Amewasihi wenzake kutoingiza siasa katika dini kwani masheikh wanaweza kufanya  kazi yao ya kuwaelimisha waumini wao na wanasiasa kutumia majukwaa yao kunadi Sera zao ili mwananchi achague kiongozi atakaeleta maendeleo ya nchi yao.

Ameongeza kusema kuwa endapo watachaguliwa kuingia madarakani watahakikisha wanaendeleza miradi yote mikubwa iliyoanzishwa na serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia awamu ya saba chini ya Rais Dkt Ali Mohammed Shein ingawa wapo watu wanaobeza miradi hiyo.

Nae Mgombea mwenza wa chama cha Ada ya Tadea kutoka Dar-es salama Hassan Konel Kijogoo  amewataka wananchi kuendeleza amani ya nchi yao na kuwaomba vyombo vya ulinzi kuwa makini kwa baadhi ya watu anaowavisha fulana ya vyama vyengine ili kuweza kuhujumu na kuwaomba kuwachukulia hatua kwa watakaokiuka sheria za nchi.

Sambamba na hayo Baadhi ya Viongozi mbali mbali wanaogombea nafasi za uongozi katika Ubunge ,Uwakilishi na Udiwani katika chama hicho amewahimiza  wananchi kuendeleza amani na utulivu wa nchi na kuwaomba kuwachagua katika nafasi zao ili kuweza kuwaletea maendeleo katika nchi yao.

Story na Rauhiya Mussa Shaaban.

Chanzo: zanzibar24.co.tz