Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT yapinga ununuzi wa ndege

ATCL ATC ACT yapinga ununuzi wa ndege

Mon, 11 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo, kimekosoa hatua ya Serikali kulipia ndege mpya tano, wakati ambao wananchi wake wanakabiliwa na ukali wa gharama za maisha, kikisema uamuzi huo unaongeza chumvi kwenye kidonda.

Katika hotuba yake bungeni jijini Dodoma, Aprili 8, mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitangaza uamuzi huo wa Serikali ili kuliboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

"Hadi Februari 2022 Serikali imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano mpya. Kati ya hizo moja ni Boeing 787-8 Dreamliner, mbili ni Boeing 737-9 moja ni De havilan-8-Q400 na nyingine ya mizigo aina ya Boeing 767-300F," amesema

Akizungumza leo Aprili 11, 2022 mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi za Chama hicho, Msemaji wa Kisekta Ofisi ya Waziri Mkuu, Dorothy Semu, amesema uamuzi huo ni ishara ya serikali kutojali changamoto iliyopo.

Katika mazingira yaliyopo, amesema haikupaswa serikali kutoa mabilioni ya fedha kununua ndege ilhali wananchi wake hawana uwezo hata wa kukabili bei ya sukari, mafuta ya kupikia, mchele, maharage na bidhaa nyingine.

"Hii imeongeza chumvi kwenye vidonda na inaonyesha kuwa serikali ipo 'out of touch' (hauguswi) na kujali," amesema Dorothy.

Advertisement Katika hatua ya kupunguza gharama za maisha, ameielekeza serikali kubana matumizi yake na kupunguza kodi katika mafuta ya dizeli kwa angalau Sh 500 kwa lita moja.

Pia, ameitaka kupunguza ushuru wa forodha kwa mafuta ya kupikia na sukari ili kupunguza bei za bidhaa hizo kwenye masoko.

Kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, Dorothy amesema haikuwapa matumaini wananchi na kugusa haja zao, ikiwemo hali ya siasa nchini, takwa la Katiba mpya, ukali wa gharama za maisha na majanga ya kuungua masoko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live