Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT wazalendo waipa tahadhari CCM Zanzibar

77761 Pic+act

Mon, 30 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe ametoa tahadhari kwa CCM Zanzibar kuwa wajindae kuondoka madarakani mwaka 2020 kwani chama hicho kimejipanga kuchukua dola.

Zitto amesema kwa nguvu iliyojengwa na chama hicho visiwani humo wana uhakika katika uchaguzi mkuu ujao wanakwenda kuitoa CCM madarakani.

Zitto ameyasema hayo leo wakati akihutubia kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho iliyokutana jijini Dar es Salaam.

Amesema chama hicho kwa sasa kinaongoza miongoni mwa vyama vilivyoimairika na nguvu hilo linawapa nguvu kuwa wanakwenda kuchukua serikali.

“Niwatumie salamu CCM Zanzibar kwamba tunakwenda kuchukua dola, najua wao bado wanahangaika nani agombee, sasa hata waje na wagombea wao 10 sisi mgombea wetu mmoja tutawapiga,”

Chanzo: mwananchi.co.tz