Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT wataka mkataba wa bandari urejeshwe bungeni

Kk Pic Act Wazalendo ACT wataka mkataba wa bandari urejeshwe bungeni

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazalendo, kimeitaka Serikali kuurejesha bungeni mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), kikisema bado kuna kasoro na upungufu unaohitaji kufanyiwa marekebisho.

Kimetaja kasoro na upungufu huo ni haki ya upekee ya kuendeleza na kusimamia bandari, kikisema ibara ya 5(1) ya mkataba huo kinatoka haki ya kampuni ya DP World kuendeleza na kusimamia, kuendeleza miradi yote kama ilivyotajwa katika makubaliano.

Chama hicho, kimesema kasoro nyingine muda wa makubaliano na usitishaji wa makubalino, kikisema IGA haijataja muda wa ukomo.

Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo (Bara), Dorothy Semu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 4, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu msimamo wa chama hicho na sakata la uwekezaji wa bandari.

"Baada ya kufanya uchambuzi wetu wa kina ACT- Wazalendo tunasema mkataba huu ufanyiwe maboresho kwa kurudishwa bungeni ili uwe na tija na manufaa kwa Taifa," amesema Semu.

Hata hivyo, Juni 10 mwaka huu, Bunge lilipitisha azimio la kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai wenye lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Mkataba wa uendelezaji na uboreshaji wa bandari baina ya Tanzania na Dubai, ulioingiwa Oktoba 25, 2022.

Serikali hizo mbili ziliingia makubaliano katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi na uendeshaji wa bandari.

Semu amesema jambo hilo lina nia njema lakini kwa namna lilivyowekwa katika mkataba linaibana Serikali Tanzania peke yake ya kuwa wajibu wa kutofanya ushirikiano na mshirika mwingine kuhusu uendelezaji wakati DP World haijabanwa.   

"Mapendekezo yetu ACT - Wazalendo IGA ifanyiwe marekebisho au kuondoa kabisa kipengele cha upekee au kuipa haki Tanzania kuhusu DP World kwa kuweka sharti hilohilo kwa mwekezaji kutofanya mazungumzo au uwekezaji na bandari shindani.

"Kuhusu kutotaja ukomo katika IGA kunahalalisha maoni ya kwamba mkataba huu ni wa muda mrefu au wa milele jambo linaloleta taharuki kwa Watanzania. Ni lazima makubaliano yawe muda mahsusi kama yaliyovyo makubaliano mengine hili lilipaswa kutajwa katika IGA," amesema Semu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live