Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT wakoshwa na kasi ya Majaliwa

Majaliwa Netbball.jpeg ACT wakoshwa na kasi ya Majaliwa

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha ACT Wazalendo Mkoa Kigoma kimepongeza hatua ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda tume na kamati mbalimbali kufuatilia tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za serikali kwenye hamashauri mbalimbali nchini ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema Mjini viongozi wa chama hicho walisema kazi inayofanywa na Waziri Majaliwa haina budi kuungwa mkono na Watanzania wote.

Akizungumzia kwenye mkutano huo aliyekuwa diwani wa kata ya Kitongoni, Maulid Kacheche alisema kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Majaliwa wito wake kwa serikali kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Naye Hussein Kalyango aliyekuwa diwani wa kata ya Kigoma Mjini alisema kuwa Waziri Mkuu amefanya kazi nzuri ya kuunda tume kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa Sh milioni 500 Manispaa ya Kigoma Ujiji na tayari watumishi wameanza kuhojiwa na kwamba isiishie kuwahoji bali hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live