Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT wajibu varangati zuio la maandamano Ikulu

ACTPIC 595x400 ACT wajibu varangati zuio la maandamano yao

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati maandamano ya Ngome ya Vijana wa ACT-Walendo yakishindwa kufanyika, Mwenyekiti wa Ngome hiyo Abdul Nondo amesema wanajipanga kufanya maandamano siku nyingine.

Nondo amesema maandamano hayo ya amani yalipangwa kuanzia Manzese hadi Ikulu kuonana na Rais Samia Suluhu Hasaan na kumfikishia ujumbe wa kutokukubaliana na ubadhilifu wa fedha za umma uliofanywa, kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya kila mwaka.

Aprili 5 Mwaka huu, (CAG), Charles Kichele aliwasilisha ripoti yake mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ikionyesha ubadhilifu wa mali za umma kiasi cha kuwaibua wananchi wanaotaka hatua stahiki zichukuliwe.

Nondo ameeleza hayo Jumanne Aprili 18, 2023 muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano yaliyokuwa yaanzie kwenye ofisi za makao makuu zilizopo Magomeni.

Nondo amesema kwenye kikao kile Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) aliwaambia yeye ana mawazo tofauti na maandamano hayo, kwani wanaona hatua stahiki zimeanza kuchukuliwa.

“Baada yakutueleza hivyo sisi tulimjibu RPC bado hatua stahiki hazijachukuliwa, akatupa barua ikipiga marufuku maandamano hayo lakini sisi tukasema ni lazima tuandamane kwa kuwa ni maandamano ya amani.

Mwenyekiti huyo amesema awali maandamano hayo yalipangwa kuanzia Manzese lakini baada ya Polisi kuanza kuzunguka tangu alfajiri wakaona waanzie kwenye ofisi za chama hicho hata hivyo polisi waliwazuia.

"Tunaenda kujifungia kuangalia ni namna gani yakufanya tena maandamano haya, hadi kumfikia Rais, risala hii tuliyokuwa tumpelekee ntaisoma hadharani ili kila mtu ajue ujumbe tuliokuwa tunampelekea." Amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live