Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT waibuka na hoja hii Zanzibar

ACTPIC 595x400 ACT waibuka na hoja hii Zanzibar

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT- Wazalendo, kimedai kitendo cha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kufuta kibali cha matumizi ya ardhi kwa kampuni ya Pennyroyal resolt kina madhara makubwa kwa maendeleo ya sekta ya utalii na kiuchumi.

Hayo yameelezwa na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Ismail Jussa Ladhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika uwanja wa Chwaka Mkoa wa kusini Unguja.

Aidha amesema kwamba kampuni hiyo tayari imefungua kesi nchini uingereza wakidai kulipwa fidia ya shilingi tirioli 2.5 sawa na bajeti ya mwaka mmoja ya serikali ya mapinduz ya Zanzibar.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa uwanja wa Amani Jussa amesema ujenzi unaoendelea katika uwanja huo umefanyika kinyume na sheria ya manunuzi na ushindani jambo ambalo ni kinyume na sheria iliyopitishwa na baraza la wawakilishi Zanzibar.

Chama cha ACT Wazalendo kinaenelea kutumika mikutano yake ya hadhara kukosoa serikali hasa kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa licha ya chama hicho kuwa mshirika katika serikali ya umoja wa kitaifa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live