Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo yatangaza wagombea ubunge

234bbdeaa5a4c3abb0709e3623a21342 ACT Wazalendo yatangaza wagombea ubunge

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha ACT Wazalendo kimetaja majina ya wanachama wake iliyowateua kugombea ubunge katika majimbo 198 kati ya 264 kwa Tanzania bara na Zanzibar.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu ametangaza majina hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa chama hicho kujiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Shaibu alisema, majimbo 66 ambayo chama hicho bado hakijataja majina ya wagombea likiwemo jimbo la Kawe na Temeke ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kusogezwa mbele kwa uteuzi wa wagombea.

Alisema, sababu nyingine ni kuendelea kusikilizwa kwa mapingamizi ambayo bado yaendelea kusikilizwa katika ngazi za uamuzi.

Shaibu alisema, changamoto kama hizo zikishatatuliwa watakaopitishwa na chama watatangazwa ili kuendelea na mchakato wa kuchukua fomu.

Alisema katika kuhakikisha usawa wa jinsia unazingatiwa chama hicho kimepitisha wanawake 30 kuwania nafasi za ubunge na uwakilishi.

Kati ya waliopitishwa ambao Shaibu aliwataja ni pamoja na Said Kubenea aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye anagombea jimbo hilo, na Maharagande Mbarala anayegombea jimbo la Segerea.

Upande wa Tunduru Kaskazini anagombea yeye mwenyewe haibu na kiongozi mkuu wa chama hicho Kabwe Zitto anagombea Kigoma Mjini.

Chanzo: habarileo.co.tz