Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo yashinda Ubunge Mtwambwe

Mohammed Ali Suleiman WA0004 Dk. Mohammed Ali Suleiman

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo kimelinda kiti cha uwakilishi jimboni Mtambwe lakini kimelalamikia mbinu chafu za makada wa Chama Cha Mapinduzi zilizolenga kulazimisha ushindi upande wao.

Kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika Jumamosi hii kutafuta kiongozi wa kuziba nafasi ya mwakilishi aliyechaguliwa mwaka 2020, mgombea wake, Dk. Mohammed Ali Suleiman, alitangazwa mshindi kwa kupata kura 2449.

Dk. Mohammed alimpita Hamad Khamis Hamad aliyegombea kwa tiketi ya CCM, akitangazwa kupata kura 1531.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo, Othman Khamis Othman, alitangaza kuwa wagombea washiriki katika uchaguzi huo walikuwa Said Nassor Hemed wa Chama cha Wamanchi (CUF) aliyepata kura 43 na Mohamed Masoud wa Chama cha CHAUMA aliyepata kura 22.

Taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi huyo inaonesha kuwa watu walioandikishwa kuwa wapigakura jimbo la Mtambwe ni 6098.

Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa ACT Wazalendo, Salim Abdalla Bimani amesema uchaguzi huo ulijaa visa na mbinu nyingi zilizolenga kulazimisha CCM kushinda.

Wananchi wa Mtambwe walipiga kura kuchagua Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kufuatia kifo cha mwakilishi waliyemchagua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Habibu Mohamed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live