Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo yashauri CAG kukagua fedha za tozo

Cag Kicherez ACT-Wazalendo yashauri CAG kukagua fedha za tozo

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wakati mjadala wa tozo kwenye miamala ya kibenki na mitandao ukiwa umeshika kasi nchini, Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kusitisha tozo mbambali na kuweka wazi kiasi kilichokusanywa.

Pia chama hicho kimemshauri mdhibitti na Mkakuzi Mkuu wa hesabu za Serikali (GAG) kufanya ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha zote zilizopatikana kutokana na tozo za miamala za simu.

ACT Wazalendo kimetoa wito huo ikiwa ni siku chache tangu serikali ieleze kuwa, imejenga vituo vya afya 234 kutokana na fedha za tozo ya miamala ya simu ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Septemba Mosi mwaka huu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema Serikali hadi kufikia Desemba 2020, Serikali ilikuwa imejenga hospitali za wilaya 102, vituo vya afya 487 na zahanati 1,198.

Akizungumza na wanahabari juzi Jumatatu Septemba 12, 2022 Msemaji wa Sekta ya Fedha na Uchumi Emmanuel Mvula amesema pamoja na mijadala hii, hivi karibuni pamekuwa na kilio cha wananchi juu ya mzigo mkubwa wa makato (tozo) yaliyoanzishwa kwenye miamala ya kibenki na kuendelezwa kwa tozo kwenye mitandao ya simu.

"Mwaka 2021, Serikali ilitueleza kwamba fedha za mkopo wa UVIKO-19, zilitumika kujenga madarasa, shule mpya, vituo vya afya na kuimarisha miundombinu,"amesema Mvula.

"Serikali inaacha maswali mengi inapojitokeza tena na kutueleza kwamba fedha za tozo za miamala ndio zinatumika kwa malengo yaleyale kama ya mkopo wa UVIKO-19,"

Amebainisha kuwa Serikali inapaswa kuweka wazi matumizi ya fedha hizo ili kuondoa mkanganyiko uliopo wa matumizi ya fedha zilizokusanywa kupitia tozo za miamala ya kieletroniki na fedha za mkopo wa UVIKO-19 uliochukuliwa na Serikali kutoka shirika la fedha duniani (IMF).

"Tunamshauri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha zote zilizopatikana kutokana na tozo za miamala za simu,"

"Ukaguzi huu ni muhimu sana kwani kuna mkanganyiko kuhusu matumizi ya fedha zilizopaswa kukusanywa kupitia

miamala ya simu na fedha za Mkopo wa Serikali wa kuimarisha uchumi kutokana athari za Ugonjwa wa Uviko-19 kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Aidha msemaji huyo amesema athari zitakazotokana na kulazimisha utekelezaji wa mfumo wa tozo ni kubwa kuliko malengo ya kifedha yanayotarajiwa kuvunwa na Serikali.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz