Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo yaitaka serikali kumrejeshea Fatma Karume uwakili wake

Fatma Karume Uwakili Fatma Karume, Mwanasheria

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kumrejeshea Fatma Karume uwakili wake kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kufungua ukurasa mpya wa wakisiasa.

Wito huo umetolewa na Katibu MKuu wa Chama hicho, Ado Shaibu akiwa kwenye kikao na viongozi na wanachama wa Kata ya Lilambo, Jimbo la Songea Mjini, Mkoa wa Ruvuma.

Fatma Karume alifutiwa uwakili wake Mwaka 2019 kutokana na kesi ambayo ilifunguliwa na Ado Shaibu wakati huo akiwa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo dhidi ya aliyekuwa Rais wakati huo, John Magufuli, kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladus Kilangi.

"Baada ya kuapishwa, Rais Samia aliahidi kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini na ameanza kuchukua baadhi ya hatua ikiwemo kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani.

"Dhana ya kufungua ukurasa mpya, inapaswa kutanuliwa na kuwagusa waathirika wote wa utawala uliopita. Inapaswa kuwagusa wavuvi waliochomewa nyavu zao, wakulima walioporwa korosho zao, wafanyabiashara walioporwa mitaji yao, wanaharakati na viongozi waliofungwa au kupotea," amesema Shaibu.

"Leo nina ombi maalum kwa Serikali. Ninaomba imrejeshee Fatma Karume uwakili wake. Bila kuathiri taratibu za kimahakama, nina hakika, hatua ya kumfutia uwakili wake ilitokana na msukumo wa kisiasa ili kumuadhibu kwa kesi aliyoisimamia kwa niaba yangu dhidi ya aliyekuwa Rais wa awamu wa tano.

 Kama sehemu ya kufungua ukurasa mpya, naye apewe nafasi ya kuendelea na majukumu yake ya uwakili," amesema Shaibu.

Mahakama yatengua uamuzi wa Fatma Karume kufutiwa uwakili

Chanzo: www.tanzaniaweb.live