Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo yaibua mpya kupanda bei ya mafuta

Waagizaji Mafuta Wakanusha Upotoshaji Unaosambazwa Mitandaoni.jpeg ACT Wazalendo yaibua mpya kupanda bei ya mafuta

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Msemaji wa sekta ya Nishati ACT- Wazalendo, Issihaka Mchinjita amesema sababu za kupanda kwa mafuta Tanzania zinatokana na changamoto ya sera za kikodi, kuondolewa ruzuku ya Serikali, upungufu wa dola na kushuka thamani ya shilingi.

Hata hivyo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), inasema sababu za kupanda bei hizo ni kutokana na kupanda gharama za mafuta kwa hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji wa mafuta hadi kufikia asilimia 17 kwa petroli, asilimia 62 kwa dizeli na asilimia nne kwa mafuta ya taa.

Pia, kuna uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi.

Hata hivyo, akizungumza leo Oktoba 11, 2023 katika mjadala wa Mwananchi space, ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Mchinjita amesema uhusiano wa kupanda kwa dola na bei ya mafuta inayoingia sokoni ni mdogo sana.

“Magari ya Serikali yangeweza kutumia gesi, yangepunguza matumizi ya Sh500 bilioni zinazotumika kuagiza mafuta kwa ajili ya mabasi mwendokasi, pia tungekuwa na sera inayoelelekeza kutumia gesi magri yote ya Serikali,” amesema Mchinjita.

Kwa mujibu wa Ewura, kiwango cha mahitaji ya mafuta nchini kimeendelea kupanda kila mwaka. Kwa mfano, mwaka jana Taifa liliingiza na kutumia lita bilioni nne ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kwa mahitaji ya mwaka 2021.

Chanzo: mwanachidigital