Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo walalamikia rafu uchukuaji, urejeshwaji fomu

11634 Act+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha ACT-Wazalendo kimesikitishwa na vitendo vya rafu na hujuma zinazoendelea kufanywa dhidi ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Buyungu na kata 77.

Miongoni mwa hujuma ni wagombea wa upinzani hasa wa chama hicho, kuenguliwa katika kinya'nganyiro kwa kile wanachodai siyo raia wa Tanzania.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ameeleza hayo leo Julai 17, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Amesema wagombea hao raia halali wa Tanzania lakini ameshanzwa na hatua ya idara ya uhamiaji kuwaeleza kuwa siyo raia hasa wakati wa uchaguzi.

Ado amedai vyombo dola vinatumika kuweka ndani wagombea wa upinzani kwa lengo la kuwafanya wasichukue fomu wakati mchakato huo ulipotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

"Wale wagombea wa upinzani waliofanikiwa kuchukua fomu, baadhi yao hawakufanikiwa kuzirudisha kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuporwa wakati wa kuzirejesha,” amesema Ado.

"Mfano wagombea wetu wanane wa kata za Tunduma walifanikiwa kuchukua fomu lakini, idara ya uhamiaji wamewaambia sio raia. Tunajiuliza haya mambo yanatoka wapi,? amehoji

Hata hivyo, Ado amesema chama hicho kitapambana kisheria dhidi ya hujuma hizo ili kuhakikisha haki ya uraia wa wagombea hao zinapatikana.

Amesema chama hicho kimefanya tathmini ya awali ya uchaguzi na kubaini wasimamizi wa uchaguzi huo na wasaidizi wanafunga ofisi zao baada ya wagombea wa CCM kuchukua fomu na kuzirejesha.

"Lengo lao ni kuhakikisha wagombea wa upinzani hawapati nafasi au kurejesha fomu na matokeo yake mnasikia mtu ameporwa fomu,"

Chanzo: mwananchi.co.tz