Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo waitaka Serikali kufanya uchambuzi virusi vya corona

97717 Act Corona+pic ACT-Wazalendo waitaka Serikali kufanya uchambuzi virusi vya corona

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha ACT- Wazalendo kimeitaka Serikali ya Tanzania kufanya uchambuzi juu ya madhara ya mlipuko wa virusi vya Corona katika uchumi wa nchi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na matokeo hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho leo Jumatatu, Machi 2, 2020 kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amewaomba wajumbe kuazimia kutoa maagizo hayo kwa Serikali.

Amesema Serikali haina budi kuchukua tahadhari kwani kulingana na hali ya huduma zetu za kiafya endapo ugonjwa huo utatua nchini utakuwa na athari kubwa kwa Taifa.

“Hakuna Mtanzania ambaye ameripotiwa kuathiriwa na ugonjwa huo lakini virusi vyake vimesambaa nchi nyingi duniani na kuna maelfu ya Watanzania wanakaa China, tuwaombee kwa Mungu ili waendelee kuwa salama,” amesema.

Vilevile, Zitto amesema China ni mshirika mkubwa wa uchumi wa Tanzania katika biashara na uwekezaji na virusi vya Corona vitakuwa na athari katika uchumi hivyo Serikali inapaswa kufanya uchambuzi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na changamoto hizo.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz