Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo waingia rasmi kudai katiba, Tume ya Uchaguzi

ACT.jpeg ACT-Wazalendo waingia rasmi kudai katiba, Tume ya Uchaguzi

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kitaunganisha nguvu na vyama vya siasa rafiki ili kudai kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya, kuelekea chaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza leo Februari 22 jijini hapa katika ziara ya kujitambulisha tangu alipochaguliwa, Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Haji Duni amesema katika madai hayo watavishirikisha vyama vyenye nia njema ya kudai mabadiliko ya kweli.

"Ndugu zangu bila Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, tutakuwa tunawasindikiza CCM wakibadilishana madaraka wenyewe kwa wenyewe kila uchaguzi.

"Sasa imefika mahala tushikamane na hasa wananchi mlioko chini kudai suala hili, mabadiliko hayaanzi kwa viongozi wa juu yanaanza chini," amesema.

Aidha ameanisha mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa ni pamoja na kuundwa kwa Serikali kivuli yenye uimarishaji wa chama na usajili wa wanachama wake kwa mfumo wa kidijitali.

Katika ziara hiyo, Duni aliambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu na maofisa wa chama hicho.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano Ngome ya Vijana Taifa, Anthony Ishika ametoa rai kwa wanachama wa chama hicho kuendelea kujitokeza kujisajili katika mfumo wa kiditali unaoitwa ACT Kiganjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live