Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo waibwaga CCM Konde

ACT WAZALENDO.png Mohamed Said Issa mgombea wa ACT Wazalendo

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: Mwananchi

Mohamed Said Issa (ACT Wazalendo), ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Konde kwa kupata kura 3408.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Abdallah Said Ahmed amemtangaza leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Katika matokeo hayo, Issa amefuatiwa na mgombea wa CCM, Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 kati ya kura 3,338 zilizopigwa.

Mgombea mwingine katika uchaguzi huo Salama Khamis Omar wa CUF alipata kura 98 na Hamad Khamis Mbarouk (AAFP) akipata kura 55.

Chanzo: Mwananchi