Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo kuadhimisha miaka mitano na yatima

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar  es Salaam.  Chama cha ACT-Wazalendo  kitaadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake kwa kuwatembelea watoto yatima.

Chama hicho kilichoanzishwa na kupata usajili Mei 5, 2014 kimesema kitafanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini, kutoa zawadi kwa watoto yatima pamoja na kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa.

Akizungumza leo Jumanne Aprili 30 jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam,  Sudi Salimu amesema matukio hayo yatafanyika wiki nzima kuanzia Mei 2 mwaka huu.

“Tutatoa damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa waliopo hospitali na hii ni moja wapo ya kuonyesha upendo na uzalendo bila kujali ni wa vyama gani,” amesema.

Kwa upande wake, katibu wa jimbo la Kinondoni wa chama hicho, Aboubakary Kabambura amesema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Zanzibar Mei 5 mwaka huu.

“Siasa zinakwenda na matukio, tuache mazoea siyo kila kitu kiwe siasa, tuonyeshe uzalendo kwa jamii ambayo inatuunga mkono, isiwe kila siku majukwaani,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz