Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo: Tunataka Katiba Mpya, tume huru ya uchaguzi

Ct Pic Datajj Ismail Jussa

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT-Wazalendo, Ismail Jussa amesema chama hicho kinahitaji michakato wa Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi kwa sababu vinakwenda sambamba.

Jussa ameeleza hayo leo Jumamosi Juni 18, 2022 katika kongamano la tatu la Tume Huru ya Uchaguzi lililofanyika wilayani Songea mkoani hapa.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa ajenda ya chama hicho ya kuhakikisha mchakato huo unafikiwa ili kuelekea katika Katiba Mpya.

Katika maelezo yake, Jussa amesema, "umekuwa na maneno mengi…,kwamba ajenda ya ACT ni tume huru ya uchaguzi na hatutaki Katiba Mpya si kweli bali tunavihitaji vyote kwa pamoja. Tunahitaji mchakato Katiba Mpya uanze sasa."

"Ndio maana tumeanisha hatua sita ikiwemo kuanzisha mkutano wa kitaifa wa majadiliano ili kupata muafaka wa kitaifa katika kuelekea kupata Katiba Mpya," amesema Jussa.

Jussa amesema mambo mengine ni kufanyika kwa mapitio ya sheria ya mabadiliko ya Katiba na sheria ya kura ya maoni, majadiliano kwenye maeneo yenye changamoto hasa muundo wa muungano, nguvu na uwezo wa rais, mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mitatu mikuu.

Advertisement ‘Mengine ni kuunda tume ya wataalamu kutengeza rasimu ya Katiba Mpya itakayochukua mapendekezo ya rasimu ya Jaji Joseph Warioba na muafaka utakaopatikana kutokana na majadiliano ya Kitaifa

"Hatua nyingine ni kuitisha Bunge la Katiba pamoja na kupata kura ya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Katiba Mpya itakayopitishwa na Bunge la Katiba kama imeridhiwa," amesema.

Jussa amesema ili kupata tume huru ya uchaguzi kunahitajika kufanyika kwa mabadiliko ya msingi yatakayosaidia kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi ya Taifa na tume huru ya uchaguzi ya Zanzibar zitakazotokana na mfumo shirikishi.

"Tuna imani vyote vitapatikanalicha ya baadhi ya wenzetu kututukana na kutushambulia, lakini ACT-Wazalendo itaendelea kusimama imara wa kutaka tume huru kuelekea Katiba Mpya," amesema.

Katibu mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema wajibu wa cha siasa ni kuwasemea na kuwatetea wananchi, akisema chama hicho kitandelea na msimamao huo katika maeneo mbalimbali ili haki ipatikane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live