Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT: Serikali itekeleze ahadi Uchaguzi Serikali za Mitaa

ACT.jpeg ACT: Serikali itekeleze ahadi Uchaguzi Serikali za Mitaa

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha ACTwazalendo kimeitaka Serikali kutekeleza ahadi yake ya kutunga sheria ya kuiwezesha Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Isihaka Mchinjita kwenye mapokezi ya kumpongeza kwa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu Taifa yaliyofanyika katika ofisi ya Mkoa wa Lindi iliyopo Lindi Mjini jana.

“Tarehe 2 Februari 2024 kwenye mchakato wa kutunga Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Serikali ilileta jedwali la maboresho ili kuipa dhamana Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa na Sheria itakayotungwa na Bunge,” alisema Mchinjita

“Kwa bahati mbaya, miswada ya Tume ya Uchaguzi na Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani bado haijasainiwa na Rais kuwa sheria hadi sasa. Hatujui ni maboresho gani hasa yamepitishwa kuwa sheria. pili, hadi sasa, serikali haijaanza mchakato wa sheria iliyoahidiwa bungeni ya kuipa madaraka Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunaona dalili za serikali kupata kigugumizi katika kutekeleza ahadi yak."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live