Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT, CHADEMA WATEMBEZA BAKULI

Bb36822955db6362b8fc2049a4e4fe94 ACT, CHADEMA WATEMBEZA BAKULI

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KUPITIA ukurasa wa Twitter Zitto Kabwe ameandika, “Safari ya kurejesha maisha ya raha na furaha imeanza, karibu na wewe ushiriki" na aliweka namba za simu na akaunti ya benki kwa wale watakaotaka kuwachangia, watume michango yao humo

Wakati ACT kupitia Kiongozi wake, Kabwe Zitto ikiomba mchango huo kwa wadau, jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia mgombea wake wa urais, Tundu Lissu kiliwasihi Watanzania wawachangie nao ili kuendesha kampeni vizuri.

Lissu amesema kwa upande wa urais, alijaza fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwamba anatarajia kutumia Sh bilioni 17 kiwango cha juu kabisa cha gharama za kampeni kwa nafasi ya urais huku akigoma kueleza wao Chadema waliweka bajeti ya kiasi gani lakini akasema fedha hizo hana.

Chanzo: habarileo.co.tz