Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

44 walisaka jimbo la Majimarefu

10847 Maji+pic TanzaniaWeb

Wed, 8 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Korogwe. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweka bayana majina ya makada wake 44 waliorejesha fomu za kuwania ubunge wa jimbo la Korogwe Vijijini akiwamo mtoto wa marehemu Stephen Ngonyani (Profesa Maji Marefu).

Profesa Majimarefu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, alifariki dunia Julai 2 mwaka huu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Pia wamo makada wa CCM, Mkurugenzi wa halmashauri na ofisa tawala.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na katibu wa CCM Korogwe Vijijini, Suraiya Kangusu kati ya waliorejesha fomu ni pamoja na mtoto wa marehemu Profesa Maji Marefu, Thomas Ngonyani.

Thomas pia ni diwani wa kata ya Kilole Wilayani hapa.

Wengine waliorejesha fomu za kuwania ubunge huo ni Jumanne Shauri ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Korogwe Mjini, John Nyika, aliyewahi kugombea ujumbe wa halmashauri ya CCM mkoa wa Tanga na ofisa tawala wa Korogwe, Michael John.

Madiwani wengine waliochukua fomu za ubunge na kurejesha ni Seif Hillary wa kata ya Mashewa na Shebila Iddi Shebila kata ya Kerenge.

Makada wengine waliorejesha fomu kuomba ridhaa ya CCM kuingia katika kinyang'anyiro hicho ni Allan Michael Bendera, Kallaghe Yusuph, Lucy Mganga, Mwanaidi Kihamia  Hemed Chanika, Issa Kiango na Nassoro Hemed 'Malingumu'ambaye ni mwenyekiti wa CCM Korogwe vijijini.

Wengine ni Bendera Shekigenda, Rose Jally, Ramadhani Mohamed, Dk George Kinyashi, Yahaya Calamba na Shwaibu Mwanyoka.

Katibu huyo aliwataja waliochukua fomu na ambao hadi muda uliopangwa kumalizika hawakujitokeza kuzirejesha kuwa ni Aweso Mandondo wa kata ya Magoma mwanaCCM Hadija Mshahara na Hoza Shehoza Hoza.

Kwa mujibu wa maelezo ya katibu huyo ni kwamba mchakato utakaofuatia ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Korogwe Vijijini kuketi Alhamisi ili kupiga kura za maoni na baadaye vitafanyika vikao vya uchambuzi kabla ya majina hayo kupelekwa ngazi ya mkoa wa Tanga.

"Katika mkutano wa kura za maoni utakaofanyika leo tumeagiza kila aliyerejesha fomu aje mwenyewe na si kutuma mwakilishi kwa sababu huu ni mchakato muhimu katika chama chetu,"amesema Suraiya.

Soma Zaidi:

Mbunge Majimarefu afariki dunia

Magufuli amlilia Majimarefu, asema alikuwa rafiki wa watu

 

Chanzo: mwananchi.co.tz