Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

41 warejesha fomu kuwania udiwani, 29 wapita bila kupingwa

Thu, 6 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wagombea 29 kati ya 32 wa udiwani wamepita bila kupingwa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Juni 5, 2019 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusainiwa na mkurugenzi wa uchaguzi, Dk Athuman Kihamia  inaeleza vyama vya siasa 14 vimeweka wagombea katika chaguzi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kati ya wagombea 41 waliorudisha fomu, 29 wamekidhi vigezo na kupita bila kupingwa.

Kihamia amesema wanachama wengine watano  hawakuteuliwa kugombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurejesha fomu za uteuzi nje ya muda, kukosa uthibitisho wa malipo ya dhamana na  kuwa na idadi pungufu ya wadhamini. 

Amesema  wagombea watano wa udiwani waliwekewa pingamizi kwa kusababisha wawili kuenguliwa  katika orodha ya wagombea udiwani. 

Chanzo: mwananchi.co.tz