Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zungu awaponda wanaume wapenda michepuko

9965 PIC+ZUNGU TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan  Zungu amewataka wananchi wilayani Ilala mkoani hapa kuacha michepuko kwa maelezo kuwa ni chanzo cha kuwa masikini.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 3, 2018 wakati akizungumza na wanawake wa mtaa wa Karume  waliohudhuria semina ya ujasiriamali iliyotolewa na Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam katika ukumbi wa Lamada jijini hapa.

"Mambo ya michepuko acheni, anayekupenda akuoe, akifanya hivyo hata baraka zinafunguka. Mambo yasiyo ya maadili kama michepuko ndiyo yanaleta ufukara miongoni mwa watu hususan vijana," amesema Zungu.

“Sisi wanaume ni waongo sana neno I love you (nakupenda) tunawaambia watu hata 20 kwa siku.”

Amewahimiza  wanawake kupendana, kupangilia biashara zao na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima akitolea mfano sherehe za siku ya kuzaliwa, kwamba  wanatakiwa kufanya wenye uwezo si kwa fedha ya mkopo.

“Kuna mama mmoja alinipigia simu ananiambia amekwama nauli ya kurudi Dar es Salaam yupo Karatu alikwenda kununua vitunguu, niliona ajabu kwani mtu lazima upangilie safari yako mapema,” amesema Zungu na kushangiliwa na wanawake wengi waliohudhuria semina hiyo.

Amesema kati ya Sh46bilioni zilizokusanywa katika manispaa ya Ilala, Sh4.5bilioni ni kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake na wenye ulemavu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo.

Naye meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Unguja na Pemba, Badru Idd amesema benki hiyo itaendelea kuwajumuisha Watanzania katika huduma rasmi za kifedha ili waweze kunufaika vizuri na mikopo hiyo ya halmashauri ambayo imewekwa kisheria.

Chanzo: mwananchi.co.tz