Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zifahamu dalili za ugonjwa mpya wa kutokwa damu puani

UGONJWA WA AJABU M Dk. Aifello Sichwale

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya kupitia kwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifello Sichwale imethibitisha vifo vya Watu watatu ambao wamefariki kutokana na kuugua maradhi mapya ambayo bado hayajulikana jina lake wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

"Dalili wanazozipata wananchi (wanaotokwa damu puani Lindi) ni homa kali, mwili kuchoka, kupata shida ya kupumua na kutoka damu puani, timu yetu ndiyo inafuatilia ili kujua kisababishi ni nini.

"Timu iliyoenda Lindi ni kutoka idara ya magonjwa ya dharura na majanga, idara ya kinga na kitengo cha magonjwa ya mlipuko, Mkemia Mkuu wa serikali wameenda kuungana na timu ya mkoa na idara ya mifugo, tuendelee kuwa na subira.

“Timu inaendelea na ufuatiliaji wa Sampuli za awali zilizopimwa katika maabara ya Taifa zimeonesha majibu hasi (negative) kwa ugonjwa wa Ebola, Marburg na Covid-19.

“Tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi wa kiepidemiolojia na kitabibu pia tunasubiri matokeo ya vipimo zaidi vya maabara ya magonjwa ya Binadamu, Wanyama na Mkemia Mkuu wa Serikali.

"Wananchi waendelee kuwa watulivu, serikali inalifanyia kazi jambo hilo ila mtu yeyote mwenye dalili hizo (mwili kuchoka, shida ya kupumua na kutoka damu puani) afike kwenye kituo cha huduma apate huduma stahiki," amesema Dkt. Aifello Sichwale, Mganga Mkuu wa Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live