Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar yapata Sh230 bilioni za kupambana na Corona

0be08989 002b 401e A0c1 A2b19bedb6ee Corona World 4a321e62 586x394 478x394 Zanzibar yapata Sh230 bilioni za kupambana na Crona

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Jamal Kassim Ali amesema Zanzibar imepata Sh230 bilioni kati ya Sh1.3 trilioni zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Uviko-19.

Jamal ametoa kauli hiyo leo Jumapili, Oktoba 10 2021 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Amesema mapambano dhidi ya ugonjwa huo hayalengi katika chanjo tu bali kuhakikisha pia kunakuwa na majisafi ili kuwawezesha watu kunawa mikono.

Pia amesema fedha hizo zitatumika katika elimu ili kuwawezesha wanafunzi wasome kwenye madarasa yasiyo na msongamano.

Jamal amesema kuwa sekta ya utalii ambayo inategemewa na watu wengi iliathirika na ugonjwa huo kwa muda wa mwaka mmoja na itapewa kipaumbele katika fedha hizo.

Amemuahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa watazisimamia fedha hizo ili zilete tija kwa kuwa na thamani ya fedha.

Chanzo: mwananchidigital