Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar haina wagonjwa wa Uviko-19

Uviko Mwinyi Pic Data Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Serikali ya Zanzibar imeeleza kuwa hivi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa ugonjwa wa uviko19 lakini haiwezi kusema ugonjwa huo umeisha visiwani hapo kwa kuwa huzuka na kupotea.

Hayo yamelezwa na Rais Dk Hussein Mwinyi leo Februari 16, 2022 wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari, Ikulu Zanzibar ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia kuanza kutumika kwa teknolojia mpya ya kupima Uviko19 kwa muda mfupi kwa kutumia simu (EDE) pamoja na kurejea kwa safari za ndege za mashirika kutoka umoja wa falme za kiarabu (UAE). 

"Kwa Zanzibar sasa maambukizi yapo chini, kipimo cha ugonjwa ni kuangalia wagonjwa waliopo hospitali kwa sasa hatuna hata mmoja aliyelazwa. Kwa ufupi Zanzibar iko salama," amesema Rais Mwinyi huku akisema kuwa kasi ya watu kuchanja chanjo ya Uviko19 ni ndogo kuliko Serikali inavyotamani.

Kwa upande wake Waziri wa Afya visiwani huo Nassor Mazrui amesema tangu Januari mwaka huu Zanzibar haijaripoti kisa kipya cha Uviko-19 kwa wakazi wala wageni lakini haitoshi kusema kuwa ugonjwa huo umeisha.

"Hatuwezi kutangaza kuwa maambukizi yameisha visiwani Zanzibar labda tukikaa kama mwaka hivi bila kuwa na kisa kipya, Kila mtu angetamani kutangaza kuwa ugonjwa huo umeisha kwake lakini ni mapema kusema," amesema Mazrui

Chanzo: www.mwananchi.co.tz