Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya chanjo milioni 40 za COVID-19 kuteketezwa

Chanjoopicc Data Zaidi ya chanjo milioni 40 za COVID-19 kuteketezwa

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya chanjo milioni 40 za Uviko-19 zinaweza kuteketezwa Afrika Mashariki, wakati mapambano dhidi ya virusi vya ugonjwa huo yakipungua.

Mpaka sasa Wizara ya Afya Uganda imeripoti kubakiwa na chanjo milioni 13.4 ambazo zinakwisha muda wake, huku Kenya ikisalia kutoa chini ya dozi 200 kwa raia wake kwa siku.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), katika nchi saba za ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania pekee imefanikiwa kutumia dozi milioni 39 kwa kufanikiwa kuchanja asilimia 53.4 ya Watanzania wote.

Rwanda na Uganda zimeshatoa jumla ya dozi milioni 26, Kenya milioni 23, Congo milioni 13, South Sudan dozi milioni 3 na Burundi imechanja dozi 35,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live