Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaidi ya 100,000 wapata Chanjo ya UVIKO-19 Tanzania

1550b243810e9c8b01b7066e03bae1bf.jpeg Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi.

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATU 105,745 kati ya walengwa 164,500 waliojiandikishwa kwa hiari kupata chanjo wamechanjwa hadi kufikia Agosti 7, 2021 kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi.

Akitoa tathimini ya maendeleo ya usambazaji na utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi, Profesa Makubi ametaka watoa huduma wasiweke vikwazo vyovyote kwa makundi lengwa kupata chanjo hizo za J&J.

Serikali ilisambaza zaidi ya dozi 1,008,400 katika mikoa 26. hatahivyo, Prof. Makubi ameelekeza viongozi katika ngazi ya serikali za mitaa wasaidie kuwatambulisha walengwa hasa wazee.

Amesema Serikali pia inaendelea na zoezi la kufuatilia maendeleo kwa watu waliopatiwa chanjo ya UVIKO 19 na pia kadi maalumu za kielektroniki zitakazo kuwa na vigezo vya kimataifa vya uthibitisho wa kupata chanjo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz