Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatoa msaada Bugando

86428 Pic+yanga Yanga yatoa msaada Bugando

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WAKATI  Yanga ikijiandaa kushuka uwanjani leo Ijumaa jioni kukipiga dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi Kuu, uongozi wa Klabu hiyo umetumia muda wao kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Rufani Bugando jijini hapa. Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, David Luhago na Afisa Mhamasishaji Anthonio Nugazi, wanachama pamoja na mashabiki wao waliwatembelea wagonjwa hao na kuwapa maneno ya faraja. Uongozi wa Yanga ulitoa baadhi ya vitu ikiwa ni sabuni, taulo za kike100, sukari, mikate na juisi huku ishu ya magodoro 30 waliyokuwa wakabidhi yakibadilishwa na sasa itatolewa pesa taslimu. Nugaz amesema kutokana na Klabu kuwa ya wananchi wameamua kutenga muda na kile walichojaaliwa kuwafariji wagonjwa. Amesema kutokana na changamoto waliyopewa hospitalini hapo ikiwamo gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa, wanaenda kulifanyia kazi na kufafanua kuwa badala ya kukabidhi magodoro 30  sasa watafanya hesabu na kuwasilisha kiasi cha pesa taslimu. Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Hospitali hiyo, Lucy Joseph amesema msaada huo utasaidia hata wagonjwa na kuwaomba wadau wengine wenye kuguswa wajitokeze. Amesema Bugando inapokea aina yoyote ya msaada bila kujali na kwamba changamoto ziko nyingi hivyo yeyote aliye tayari anakaribishwa kwa kufuata utaratibu. Naye Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi hospitalini hapo, Ester Pastori amesema moja ya changamoto kubwa ni upungufu wa vifaa tiba na gharama kwa wagonjwa. Amesema wagonjwa wengi wanashindwa kumudu gharama za matibabu lakini vifaa tiba kuwa na gharama kubwa, hivyo mahitaji makubwa ni pesa.

Chanzo: mwananchi.co.tz