Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yaliyoshuhudiwa Hospitali Zakhiem

47424 PIC+ZAKIEM

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar er Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile, ameonyeshwa kutoridhishwa na utendaji wa Hospitali ya Mbagala Zakhiem kutokana na dosari mbalimbali.

Katika ziara ya kushtukiza hospitalini hapo jana, Dk Ndugulile alionyesha kusoma mchezo mchafu unaohusisha dawa ambako wagonjwa wanaambiwa zimeisha ilhali zimejaa stoo.

Dk Ndugulile alisema alipata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ukosefu wa dawa katika hospitali hiyo na ameshangaa kukuta chumba cha kuhifadhi dawa kimejaa.

“Naona kuna mchezo mchafu hapa, watu wanaambiwa hamna dawa halafu zimejaa stoo, natoa maelekezo kuanzia sasa kila mwanzo wa wiki andaeni orodha ya dawa zinazopatikana wawe nayo wanaoandikia wagonjwa,” aliagiza.

Malalamiko mengine aliyokutana nayo Dk Ndugulile ni uchache wa wataalamu hali inayosababisha msongamano na wahudumu kutoa kauli mbaya kwa wagonjwa.

Alipofika hospitalini hapo, alishuhudia idadi kubwa ya watu wakingoja huduma huku ikionekana watoa huduma wamezidiwa.

“Nipo hapa tangu saa 11 asubuhi mtoto wangu anaumwa hadi sasa sijamuona daktari, hali hii inakatisha tamaa,” alilalamika Mariam Semi.

Licha ya umati huo, Dk Ndugulile alishtushwa na taarifa ya mhasibu kuwa wanaingiza Sh2 milioni kwa siku. “Hivi kweli mko serious (makini) watu wote hawa waliojaa nje mnasema mapato ni Sh2 milioni pekee, kuna tatizo mahali na msifikiri nimekuja hapa kuuza sura huu ni uzembe wa wazi,” alisema.

Aliomba orodha ya vipimo vilivyofanyika Ijumaa ili aangalie kama vinaendana na kiwango walichomweleza, lakini hadi anaondoka orodha hiyo haikupatikana.



Chanzo: mwananchi.co.tz