Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yafafanua wanaopika kwa kutumia dawa za maumivu

Dawa Chakula Hatari.png Wizara yafafanua wanaopika kwa kutumia dawa za maumivu

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumiaji wa dawa za maumivu katika mapishi hususani katika kulainishia kitoweo cha nyama, wapo hatarini kuugua magonjwa ya moyo, ini na figo.

Taasisi ya Elimu ya afya iliyo chini ya Wizara ya Afya imeeleza madhara hayo ikijibu chapisho la Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile juu ya taarifa za kuogofya kuhusu baadhi ya mama lishe kutumia dawa za kupunguza maumivu katika kuivisha na kulainisha kitoweo hususani nyama ya utumbo.

"Jambo hili ni hatari kiafya kwani dawa hizi zinapopashwa moto hutoa kemikali inayoitwa Amino, inapomeng'enywa na mwili huleta madhara," imeeleza taarifa ya Elimu ya afya

Dk Ndugulile ni daktari kitaaluma, kupitia chapisho lake mtandaoni hakusita kugusia juu ya hatari ya matumizi ya dawa hizo zikichomwa au kuchemshwa.

"Athari ya dawa hizi zinapopikwa ni kubwa, ikiwa ni pamoja na kuathiri figo, ini na moyo. Elimu kwa jamii inahitajika kwenye jambo hili.

Nayo, Wizara ya Afya inaendelea kutoa wito kwa waandaji wa vyakula kuzingatia maandalizi yanayojali afya ya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live