Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara yaanika saratani tano Kanda ya Ziwa

God Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel

Sat, 12 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya imetaja saratani tano zinazoongoza kanda ya ziwa ikiwemo saratani ya kibofu cha mkojo, na kubainisha kuwa bado inafanya utafiti kujua chanzo cha ugonjwa huo.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, alisema hayo bungeni jana alipokuwa ikijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Kabula Shitobela.

Katika swali lake, Mbunge huyo alihoji serikali imefikia wapi kuhusu kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ugonjwa wa saratani katika mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa, kwa kuwa unaongoza kuwa na wagonjwa wengi.

“Je, kuna mpango gani wa kudhibiti ongezeko la ugonjwa huo?” alihoji Mbunge huyo.

Katika majibu ya swali hilo, Naibu Waziri alisema serikali kupitia wizara imeshafanya utafiti wa kina nchi nzima uliosaidia kutambua kuwa Kanda ya Ziwa ni saratani zipi zinaongoza.

Alitaja saratani hizo kuwa ni za kibofu cha mkojo, mji wa uzazi kwa kinamama, saratani ya damu, macho na figo.

Pia alibainisha kuwa wataalamu wamekusanya sampuli 7,000 za damu za watu ambao hawana saratani ili kulinganisha na sampuli za damu za wenye saratani.

Alisema utafiti huo utasaidia kubaini chanzo cha hizo saratani kwa kuwa hadi sasa bado utafiti unaendelea na visababishi vinavyosemwa bado ni nadharia tu kutokana na shughuli za kijamii katika maeneo husika.

Hadi sasa, alisema mpango wa kudhibiti ongezeko umejikita katika kutoa elimu ya afya kwa viashiria vinavyodhaniwa, pamoja na kuzingatia Mkakati wa kitaifa wenye maeneo saba yaliyoainishwa ili kudhibiti viashiria vya saratani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live