Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Afya yazitaka hospitali zote kuweka masanduku ya maoni

Wooden Suggestion Box Wizara ya Afya yazitaka hospitali kuweka masanduku ya maoni

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

atibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu amezitaka hospitali za rufaa nchini kuhakikisha zinakuwa na mfumo rasmi ambao unajulikana kwa wananchi wanaowahudumia ili kutoa mrejesho wa huduma wanazotoa.

Dkt. Jingu amebainisha hayo wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani -Tumbi kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma huduma za afya katika hospitali hiyo.

“Tukiimarisha njia za kupata mrejesho kutoka kwa wananchi tunaowahudumia itasaidia kujua ubora wa huduma tunaotoa upo kiasi gani kwani jukumu la hospitali za rufaa ni kutoa huduma kwa viwango vya juu,” ameieleza Dkt. Jingu

Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji wa kutosha katika sekta ya afya hivyo ni jukumu la wataalamu wa afya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kunufaika na uwekezaji huo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumain Nagu ametoa wito kwa wataalamu wa afya kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia Watanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live