Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Afya yatoa majokofu 17 kuhifadhi chanjo

Wizara ya Afya yatoa majokofu 17 kuhifadhi chanjo

Sat, 30 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Buchosa. Wizara ya Afya nchini Tanzania imetoa majokofu 17 ya kutoa chanjo kati ya vituo 36 vinavyotoa huduma hiyo Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Novemba 30, 2019 na Waziri wa Afya,  Ummy Mwalimu wakati akizindua majokofu ya kuhifadhi chanjo kwenye zahanati ya Nyakasungwa.

Amesema Serikali inasogeza huduma kwa wananchi, itaendelea kufanya hivyo hadi vituo vyote vipate majokofu hayo.

Ummy amewataka wahudumu wa afya kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kauli nzuri zitakazowapa wagonjwa matumaini na kuwataka wahudumu wa afya kuyatunza majokofu hayo.

Moshi Shabani  mkazi wa kijiji cha Nyakasungwa ameishukuru Serikali kwa kutoa vifaa hivyo vitakavyoimarisha utoaji wa chanjo.

Chanzo: mwananchi.co.tz