Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wizara ya Afya yafuatilia taarifa kuugua watoto

E368af35106c7666b7c7f6a9a13479ff Wizara ya Afya yafuatilia taarifa kuugua watoto

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema wanafuatilia taarifa za kuwepo ugonjwa wa mafua kwa watoto nchini kupitia wataalamu wa epidemiolojia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, amesema taarifa rasmi zitatolewa siku mbili zijazo.

“Ufuatiliaji unafanyika hapa Dar es Salaam, kwa hiyo tutapata taarifa, lakini ni kweli tulisikia hizo tetesi za watoto kuugua mafua, huwezi kukurupuka kusema tuna mafua haya.

“Tutataliongelea baada siku mbili, baada ya timu kukamilisha tutapata taarifa vizuri, hata hivyo kuna tetesi tumepata kwamba Uganda kuna aina fulani ya mafua na tumepata Dar es Salaam kuwa kuna watoto,” ameeleza.

Amewahimiza Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaopata mafua wanachukuliwa sampuli, ili iwe rahisi kuwagundua.

"Kama hawajapima ni vigumu kujua ni mafua ya aina gani ,"amesisitiza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live