Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wito watolewa kutokomeza Kifua Kikuu

Kifua Kikuu.jpeg Wito watolewa kutokomeza Kifua Kikuu

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kifua Kikuu (TB) ni moja ya sababu kuu za vifo barani Afrika. Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika (AU), ugonjwa huo unaua mamia kwa maelfu ya watu kila mwaka.

Viongozi wa Umoja wa Afrika wamesema hayo katika mkusanyiko wa kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani 2024, ambayo huadhimishwa Machi 24 kila mwaka ili kuongeza welewa wa watu kuhusu ugonjwa huo hatari. Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya AU jijini Addis Ababa Ethiopia chini ya kaulimbiu ya “Ndio! Tunaweza kutokomeza TB. "

Sheila Shawa, mtaalamu mkuu wa masuala ya kiufundi wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) amezungumzia suala hilo akisema: "Takwimu zinazorota kupungua kutokana na Afrika kubeba mzigo mkubwa wa asilimia 23 ya mzigo wote wa ugonjwa wa TB duniani. Zaidi ya asilimia 33 ya vifo vya TB vinatokea barani Afrika." Ndio! Tunaweza kutokomeza TB

Amegusia ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inayofichua kuwa takriban watu milioni 2.5 waliugua TB barani Afrika na kusababisha vifo vya watu 424,000 mwaka 2022 na kuongeza kuwa, ugonjwa wa TB ndio uliosababisha vifo vingi zaidi barani Afrika mwaka uliofuata.

Amesema, watu wanaoishi katika mazingira magumu kama vile watoto na mabarobaro wanaweza kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata TB hasa wakati mfumo wao wa kinga unapokuwa umeathiriwa na utapiamlo, VVU au magonjwa mengine sugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live