Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wito- Kila mmoja achukue tahadhari ya ugonjwa wa Ebola

89371 Ebola+pic Wito- Kila mmoja achukue tahadhari ya ugonjwa wa Ebola

Fri, 20 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuikabili nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Watanzania wameendelea kusisitizwa kuchukua tahadhari ya namna ya kutambua mgonjwa na jinsi ya kujinga pindi utakapoingia nchini humo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Desemba 20, 2019 katika semina ya kujenga uelewa dhidi ya ugonjwa wa Ebola iliyohusisha viongozi mbalimbali wakiwamo wa dini, maofisa afya, vyombo vya habari, wakurugenzi iliyoandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Shirika la Msalaba Mwekundu (Red cross).

Dk Ndeniria Swai ambaye ni mratibu wa tafiti za mkoa wa Dar es Salaam amesema licha ya ugonjwa wa Ebola kutoingia nchini humo, jitihada zinahitajika za makusudi kuwaelimisha wananchi kutambua na kujikinga na ugonjwa huo.

“Tumeamua kuendelea kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao haujaingia Tanzania lakini majirani zetu kama Kongo ambao tuna mwingiliano mkubwa wao ni ugonjwa huu uko kwao,” alisema Dk Ndeniria ambaye pia ni msimamizi wa uelimishaji wa ugonjwa wa Ebola mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kupitia mafunzo hayo yanayohusisha watu wa kada mbalimbali yatasaidia kwa kiasi kikubwa na wao kwenda kuyatoa kwa watu wanaowaongoka mathalani viongozi wa dini, wakurugenzi, wakuu wa wilaya na wasanii wanaoweza kutunga nyimbo za kuelimisha kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Ofisa tathimini na ufuatiliaji wa Ebola Tanzania kutoka Redcross, Saimon Kadogosa amesema jamii inapaswa kuwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo.

">Amesema Redcross imekuwa ikishiriki katika majanga mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali ili kuifanya jamii kuwa na uelewa kwa mambo kadhaa ikiwamo hilo la Ebola.

Naye Oscar Kapera ambaye ni Ofisa kutoka wizara ya afya kitengo cha elimu ya afya kwa umma amesema wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kwa "kujua ni njia gani ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola kwani kinga ni bora kuliko tiba."

"Tunatoa elimu kwa njia mbalimbali hasa vyombo vya habari na wahudumu wa afya ngazi za jamii, walimu shuleni wamekuwa wakikutana na wananchi kwenye mikusanyiko ili kutoa elimu ya utayari," amesema

Kapera ametaja mikoa kumi ambayo iko katika hatari ya kupata ugonjwa huu kutokana na mazingira yake kuwa ni; Dar es Salaa, Kigoma, Katavi,Rukwa, Sogwe, Dodoma, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill Tegeta Dar es Salaam, Richard Hananja amesema yeye ni kiongozi wa jamii, "naongoza jamii na Tanzana ya kiwanda mimi kiwanda changu ni jamii na nikipata uelewa nitakwenda kuwaeleza ili ugonjwa huu ukitokea wajue cha kufanya."

Amesema kukiwa na waumini wenye afya njema wataweza kutoa sadaka na kulipa kodi lakini kukiwa na waumini wasiokuwa na afya hata matoleo na utendaji kazi hautakuwa mzuri.

Mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Seif Mhenga amesema, “ni muhimu tena ni muhimu sana sisi kama viongozi wa dini kulipokee hili kwa mikono miwili na kulifanyia kazi.”

Mhenga amesema, “kama mwili hauna amani hata jamii haitanufaika nawe na ukiumwa hauna amani. Huu ni ugonjwa mkubwa na hatari, ni bora na ni bora zaidi kuwa kinga ni bora zaidi kuliko tiba hivyo tutatumia mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha masheikh pamoja na wale tunaowaongoza.”

Chanzo: mwananchi.co.tz