Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiki ya Maabara yapima 3000 Mwanza

D138a9efb097c25e8ba0e87a6be2170d Mwenyekiti wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 3000 jijini Mwanza wamepimwa bure vipimo mbalimbali katika wiki ya wataalamu wa maabara mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya (MeLSAT) mkoani Mwanza, Bertrand Msemwa amesema hayo leo jijini Mwanza kuwa watu 3360 wamepimwa kuanzia Mei 2 hadi 6, mwaka huu.

Amesema waliojitokeza walipimwa maradhi ya shinikizo la damu, homa ya ini , kisukari, Virusi vya Ukimwi (VVU), kaswende, malaria na Virusi vya corona (Uviko-19).

Amesema waliogundulika kuwa na homa ya ini ni asilimia 4, Uviko- 19 asilimia 12, kaswende asilimia 5.4, VVU asilimia 2.1 na malaria asilimia 0.9.

Amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao na kuendelea kuchukua hatua dhidi ya tatizo la Uviko 19, kwani bado lipo katika eneo hilo.

“Tunatoa wito kwa serikali kuwaajiri vijana waliohitimu masomo hayo, kwani bado maeneo mengi ya huduma za afya hapa nchini kunahitajika watumishi hao,” amesema Msemwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike, amesema kuwepo wataalamu hao katika maeneo yote yanayotoa huduma za afya ni mhimu, ili kuwezesha wagonjwa kupata matibabu ya uhakika kwa maradhi yanayowasibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live