Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye uvimbe kwenye kizazi kutibiwa bila upasuaji Muhimbili

62715 Muhimbilipic

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Radiolojia Hospitali ya  Taifa ya Muhimbili (MNH),  Dk Frola Lwakatare amesema wanawake wenye  uvimbe kwenye kizazi watapatiwa matibabu bila kufanyiwa upasuaji kama ilivyokuwa awali.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 14, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu programu ya mafunzo ya tiba ya radiolojia itakayofanyika kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Emory na Yale vya Marekani  na hospitali ya Buffalo New York ikiongozwa na kuongozwa na Dk Janice Newsome.

Amesema awali wanawake wenye uvimbe walikuwa wakifanyiwa upasuaji, kwamba kwa sasa watakuwa wakiingizwa mpira yenye chembechembe maalumu kwenye mishipa ya damu ambayo itaziba mishipa inayopeleaka damu kwenye uvimbe.

"Baada ya mishipa hii kuziba uvimbe unakosa damu  au chakula chake na kusinyaa na kufa kabisa. Mwanamke mwenyewe uvimbe kwenye kizazi endapo akipatiwa tiba hii hakuna haja ya kumfanyia upasuaji wa kuondoa uvimbe.”

"Tiba hii itamsaidia mgonjwa kurudi haraka nyumbani na kufanya shuguli zake baada ya kupata matibabu. Nawaeleza  Watanzania Muhimbili imejipanga vizuri katika suala hili " amesema Dk Lwakatare.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz