Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye kadi NHIF kupima bure homa ya dengue

56826 Pic+nhif

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Wakati Serikali ya Tanzania ikiweka utaratibu maalum kwa wananchi kupata huduma ya kipimo na matibabu ya homa ya dengue, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema wateja wa mfuko huo wameanza kupata huduma hiyo bure.

Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa Mei 10 na kitengo cha mawasiliano NHIF imeeleza kuwa, kutokana na Sheria ya Afya ya Umma ya mwaka 2009, Serikali imeweka utaratibu kwa wananchi wote ikiwamo wateja wa mfuko huo wenye dalili za ugonjwa huo kupata huduma bila malipo katika vituo vya umma vilivyoainishwa ikiwamo hospitali za rufaa za mikoa.

“Mfuko unawasihi wanachama wake wote kuzingatia maelekezo ya kujikinga na kudhibiti mbu wanaoeneza ugonjwa huo kama yalivyotolewa na wizara ya afya, Mmendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto,” imesema.

Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza mfuko kuwa, kwa kushirikiana na hospitali za umma katika mikoa iliyoainishwa, unaandaliwa utaratibu kwa wanachama wake kupata huduma ya kipimo cha homa hiyo katika mikoa iliyoathirika.

Hospitali hizo ni pamoja na Amana, Temeke, Mwananyamala, Mnazi Mmoja, Bombo  Tanga na hospitali ya mkoa wa Singida.

Chanzo: mwananchi.co.tz