Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye VVU wapokea vifaa vya Mil. 324

VVU MISAADA Wenye VVU wapokea vifaa vya Mil. 324

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ICAP Tanzania limekabidhi vifaa vya Sh314 milioni vya utunzaji wa taarifa kwa kutumia alama za vidole (Biometric) na ufuatiliaji wa watu wanaohudhuria kwenye vituo vinavyotoa tiba na matunzo ya Watu wanaoishi na Virusi Ukimwi (WAVIU) mkoani Mwanza.

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ICAP Tanzania, Dk John Kahemele amesema vifaa hivyo vitasambazwa katika vituo vya afya 208 vinavyosimamiwa na ICAP kwenye halmashauri nane za mkoa huo.

“Ugawaji wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi ambao ulitoa mwongozo wa kuboresha udhibiti wa taarifa za watu wanaoishi na VVU na utaondoa matumizi ya karatasi kuhifadhi taarifa zao”

Vifaa hivyo ni Kompyuta zaidi 122, vifaa vya alama za vidole (Biometric) 299, reuters za intaneti 177, zitakazosaidia kuboresha udhibiti na uhifadhi wa taarifa zao na kufuatilia mahudhurio ya matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amina Makilagi ambae ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amesema vifaa hivyo vitasaidia kuweka usiri wa taarifa za Mgonjwa tofauti na mwanzo taarifa zilipitia kwa watu zaidi ya watu wa tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live