Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Afya awajulia hali majeruhi ajali iliyoua 15 (+picha)

Mtanzanianews 131209819 215169153384044 4035217575732201166 N Waziri wa Afya awajulia hali majeruhi ajali iliyoua 15 (+picha)

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ametembelea majeruhi wawili waliopata ajali iliyohusisha gari aina ya Coaster iliyokua ikitoka Mkoani Mwanza kuelekea Itigi kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya watu 15 katika eneo la Mkiwa Wilayani Ikunga Mkoani Singida.

Pamoja na kuwajulia hali majeruhi hao ambao ni aliyekua Harusi Herry Mkamwa na ndugu yake Shakila Kassim ambao wamelazwa katika Hospitali ya St. Gasper iliyopo Itigi, Waziri Dorothy pia ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ambapo miili 14 imehifadhiwa na kushiriki ibada ya kuaga miili hiyo ambayo inatarajiwa kusafirishwa kwenda Mwanza na Mbeya.

Waziri Dorothy pia amewafariji wafiwa na kusema kuwa Serikali iko bega kwa bega katika kuhakikisha marehemu wanasafirishwa na kuhifadhiwa katika nyumba zao za milele.

Chanzo: millardayo.com