Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri wa Afya ajiuzulu baada ya mtalii mjamzito kufariki kwa kutohudumiwa

Ma Lll Waziri wa Afya ajiuzulu baada ya mtalii mjamzito kufariki kwa kutohudumiwa

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa afya wa Ureno, Dkt.Marta Temido amejiuzulu saa chache baada ya ripoti kuibuka kuwa mtalii mjamzito amefariki dunia.

Mwanamke huyo wa India mwenye umri wa miaka 34 aliripotiwa kufariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo alipokuwa akihamishwa kutoka Hospitali ya Santa Maria ya Lisbon ambayo ni hospitali kubwa zaidi nchini Ureno kwa sababu kitengo chake cha watoto wachanga kilikuwa kimejaa.

Dkt.Marta Temido alikuwa waziri wa afya wa Ureno tangu 2018, na anasifiwa kwa kuiongoza Ureno kupita janga la Uviko-19, lakini baada ya mfuatano wa matukio yanayo chafua wizara ya afya siku za hivi karibuni, serikali ilitoa taarifa kwamba Dkt Temido “ametambua kwamba hakuwa na ulazima tena wa kusalia ofisini”.

Kumekuwa na visa kama hivyo nchini Ureno katika miezi ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na vifo tofauti vya watoto wachanga wawili ambao mama zao walikuwa wamehamishwa kati ya hospitali na kushindwa kuvumilia kucheleweshwa kwa muda mrefu.

Serikali imetoa taarifa ya upungufu wa watumishi wa afya nchini Ureno hususani waliobobea katika masuala ya magonjwa ya wanawake na uzazi ambapo inafikiria kuajiri kutoka nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live