Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri ataka mjadala wa VVU kwa vijana

11193 Vvu+pic.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshughulikia wenye (ulemavu), Stella Ikupa amesema kunahitajika mjadala kujua sababu zinazofanya uwepo wa idadi ya vijana wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza na vijana wanaoishi na VVU, leo Juni 10 2018, Stella amesema taarifa za Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) zinaonyesha Tanzania imebeba asilimia tano ya vijana waliobalehe duniani wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wanaoishi na VVU.

Amesema pia taarifa za Ofisi ya Takwimu Nchini (NBS) zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya maambukizi mapya kwa vijana ni walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 24.

Amesema takwimu za viwango vya kufubaza VVU ni kidogo kwa watu wenye umri mdogo ukilinganisha na watu wazima jambo ambalo ni tishio kwa maendeleo ya Taifa.

“Inawezekana hii inasababishwa na kutotafutwa, ama kutopatiwa elimu kwa jinsi gani wanaweza wakawa wafuasi wazuri wa kutumia hizi dawa lakini pia kunahitajika kujiuliza sisi sote kwanini hali iko hivyo,”amesema.

Amesema inawezekana kuna mapungufu katika utoaji huduma kwa VVU, unyanyapaa na ubaguzi ama tofauti katika usawa wa jinsia.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, (NYP+), Fadhili Kiteve amesema mkutano huo unahusisha vijana 100 wanaoishi na VVU kutoka nchi nzima lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu juu ya changamoto zinazowakabili.

“Kama tunavyojua vijana wanaoishi na VVU wanakabiliwa na changamoto ya unyanyasaji, ubaguzi na hayo huchukua nafasi kubwa zaidi katika maisha yao, sasa wanapokutana hapa wanaweza kufahamu namna gani ya kukabiliana na changamoto hizo,”amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz