Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy kuzindua maadhimisho ya siku 16 za ukatili wa kijinsia Tanzania

Waziri Ummy kuzindua maadhimisho ya siku 16 za ukatili wa kijinsia Tanzania

Tue, 26 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Ummy Mwalimu kesho Jumanne Novemba 26,2019 atazindua maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Novemba 25, 2019 na kitengo cha mawasiliano cha Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwenye wizara hiyo imesema kilele cha maadhimisho kitakuwa Desemba 10, 2019.

Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Erasto Ching’oro amesema kauli mbiu katika maadhimisho hayo kwa mwaka 2019 ni kizazi chenye Usawa: Simama Dhidi ya Ubakaji.

Amesema lengo maadhimisho hayo ni kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa, uzoefu  kujenga uwezo wa pamoja.

Malego mengine ni matumizi mazuri ya raslimali zinazopatikana na kuunganisha nguvu za pamoja katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia.

“Katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia, wizara inawaomba Watanzania na wadau kuunganisha nguvu na kubuni mikakati ya kijamii ambayo italeta suluhisho la kudumu,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz