Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy kuhusu muswada wa sheria wa kujipima Ukimwi

83863 Pic+ummy+2 Waziri Ummy kuhusu muswada wa sheria wa kujipima Ukimwi

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania iko mbioni kupeleka bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ili kuruhusu watu kujipima wenyewe virusi vya ukimwi.

Waziri wa Afya nchini humo, Ummy Mwalimu ameeleza hilo leo Jumatatu Novemba 11, 2019 wakati akifungua semina elekezi ya virusi vya ukimwi kwa wasanii.

Ummy amesema mabadiliko hayo ya sheria yanakuja kutatua changamoto ya unyanyapaa na baadhi ya wahudumu wa afya kutotunza siri za wagonjwa.

Amesema Serikali imebaini kuna changamoto ya watu kushindwa kupima kwa kuhofia unyanyapaa na taarifa za afya zao kuanikwa.

“Kupitia mabadiliko hayo sasa sheria itaruhusu watu kujipima, tutagawa vile vifaa vya kujipimia ila baada ya kujipima tungependa pia uende kwenye kituo cha afya,” amesema

Kauli hiyo ya waziri ilipokelewa kwa shangwe na wasanii waliohudhuria semina hiyo na kueleza kusaidia kuongeza idadi ya watu wanaopima.

Msanii Banana Zoro amepongeza mabadiliko hayo ya sheria na kueleza kuwa yataibua hamasa kwa vijana kujitokeza kupima.

Naye msanii wa vichekesho, Tabu Wakutindinganya amesema uamuzi huo ni hatua kubwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Rais wa shirikisho la muziki Tanzania, Ado Novemba amesema Serikali imefanya jambo jema kuwashirikisha wasanii na kuamua kuwatumia kwenye mapambano dhidi ya ukimwi.

“Zimekuwepo kampeni nyingi wasanii wametumiwa na kuachwa tuna imani kampeni hii tutakwenda pamoja hadi mwisho na waziri wetu utakuwa pamoja nasi,” amesema Novemba

Chanzo: mwananchi.co.tz