Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy kazungumzia ahadi ya serikali kugawa gari za Wagonjwa nchi nzima

Halmashauri Pic Data Waziri Ummy kazungumzia ahadi ya serikali kugawa gari za Wagonjwa nchi nzima

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema ipo kwenye utaratibu wa kununua magari ya wagonjwa kwaajili ya halmashauri zote nchini ambapo hadi kufikia Machi 2022 mpango huo utakuwa umekamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu leo Jumatatu Desemba 6, 2021 wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kwamagome Halmashauri ya Mji Handeni baada ya kuzindua zahanati ya eneo.

Amesema kuwa kabla ya mwezi wa tatu mwakani Serikali itakuwa imeshakamilisha upatikanaji wa magari ya wagonjwa kwa halmshauri, ambazo zitaweza kusafirisha wagonjwa.

"Mpaka Machi 2022 Serikali itakuwa imeshakamilisha utaratibu wa kupatikana magari ya wagonjwa kwa halmashauri 184 nchini, lengo ni kusaidia kwa wagonjwa wanaotaka kusafirishwa iwe rahisi", amesema Waziri Ummy.

Amewataka wananchi kupuuza kauli inayotolewa na baadhi ya watu kuwa Serikali ya awamu ya sita inasitisha mfumo wa elimu bila malipo, na kudau kuwa kauli hizo sio kweli na Seikali haina mpango huo.

Mbunge wa Handeni Mjini, Reuben Kwagilwa amemuomba Waziri Ummy kuridhia zahanati ya Hedi kata ya Kwamagome aliyoizindua ipandishwe hadhi iwe kituo cha afya, kwasbabu wananchi wa eneo hilo wanatembea umbali mrefu kwenda hospitali ya wilaya.

Advertisement Amesema kuna wananchi zaidi ya 18,000 kwenye eneo hilo hivyo huduma za afya zikiboteshwa kwa zahanati yao kupanda hadhi, watapata huduma karibu.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amezishukuru taasisi zisizo za Serikaki za Amref, World Vision, Islamic Help na wadau wengine kwa kusaidia kujenga zahanati na kutoa vifaa, hali ambayo imesaidia kuboresha huduma za afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live