Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesemaTanzania inakadiriwa kuwa na wagonywa wapya 42,000 wa saratani kila mwaka ambapo asilimia 68 ya wangonjwa hao wanafariki dunia kila mwaka.
Waziri Ummy amesema hayo leo Jumapili Aprili 10, 2022 wakati wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kisasa cha matibabu ya saratani kitakachofanya kazi kwa ubia kati ya Serikali na Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa “Nimeeleza mzigo wa ugonjwa wa saratani nchini Tanzania, tunakadiriwa kuwa kuwa na wagonywa wapya takribani 42,000 wa saratani kila mwaka, katika wagonjwa hao wapya 42,000 asilimia 68 ya wangonjwa hao wanafariki dunia kila mwaka” amesema.
Waziri Ummy amesema kuwa moja ya sababu ni upatikana wa huduma ya kupima na matibabu.
“Moja ya sababu ni upatikana wa huduma ya kupima na matibabu ya saratani kwa hiyo mradio huu utatusaidia kuwafikia Watanzania wengi za kupima pamoja na matibabu” amesema
Amesema kituo hicho kikikamilika kitahudumia wagonjwa wa saratani 120 kwa siku hivyo kitaipunguzia mzigo na msongamano wa wagonjwa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).
Ametoa rai kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ikiwamo ya ugonjwa wa saratani ili wanapogundulika wapate tiba mapema
“Naumia sana kama Waziri wa Afya ninapoona takwimu katika kila watu 80 kati ya 100 ambao wanakwenda Ocean Road wakiwa wagonjwa wa saratani, tayari saratani iko katika hatua ya tatu au ya juu kabisa kwa hiyo inafanya hata matibabu yasiwe ya ufanisi” amesema
Ametaja saratani zinazoongoza nchini kuwa ni saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti ambazo zinawakumba wanawake na saratani ya tezi duma kwa wanaume.
“Tusiogope kupima saratani aina yoyote ya kipimo, kwa sababu tunasema kinga ni bora kuliko tiba, watu wakiona dalili msikae nyumbani au ukakimbilia kwa mganga wa kienyeji wakati una saratani, nendeni hospitali. Saratani inatibika ikigundulika mapema” amesema Waziri Ummy