Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ummy azindua mitambo ya Oksijeni ya Bil. 1.5 Hospitali ya Mkapa Dodoma

WhatsApp Image 2022 07 01 At 4.jpeg Waziri Ummy azindua mitambo ya Oksijeni ya Bil. 1.5 Hospitali ya Mkapa Dodoma

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amezindua mitambo wa hewa tiba ya Oksijeni wenye thamani ya bilioni 1.5 kwenye hospitali ya Benjamnin Mkapa iliyoko jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema usimikaji wa mitambo hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreshwa na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja mitambo 14 imeshasimikwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini.

"Sisi kama Sekta tumejiwekea vipaumbele vyetu ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ingependa kuviona tunavitekeleza, kipaumbele kikubwa ni ubora wa huduma za afya, hivyo mitambo hii ina lengo la kuokoa maisha kwa wananchi wake".

Waziri Ummy amesema wanatarajia kusimika mitambo mingine 57 ya hewa tiba ya Oksijeni kwenye hospitali za rufaa za mikoa,Kanda pamoja na Wilaya nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameipongeza hospitali hiyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Alphonce Chandika kwa kuhakikisha kuwa kazi ya usimikaji wa mitambo huo unakamilika kwa wakati na unazingatia viwango vinavyotakiwa

Ameongeza kuwa mitambo hiyo haitosaidia hospitali hiyo tu bali hata hospitali na vituo vya mikoa wa Dodoma na mikoa ya jirani ikiwemo Manyara, Singid na Iringa.

Pia amesema licha ya mitambo huo ambao ni mradi mmoja kati ya miradi 17 ambayo inatekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo jumla ya takribani Bilioni 10.02 zimeelekezwa katika kukamilisha miradi hiyo hospitalini hapo.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika amesema mitambo hiyo inazalisha mitungi 400 kwa siku na una sehemu mbili ambazo hazitegemeana hivyo unaweza kuwasha sehemu moja kipindi unatumia ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea wakati wote hata wakati wa matengenezo kinga inapolazimu kuzima upande mmoja.

Dkt.Chandika aliongeza kabla ya hapo hospitali ilikua ikitumia mitungi 200 kwa mwezi lakini kipindi cha UVIKO-19 matumizi yakiongezeka hadi kutumia mitungi 200 kwa siku na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa hospitali na kutumia milioni 10 kwa siku badala ya milioni 10 kwa mwezi kwa kipindi hicho cha UVIKO-19.

Bilioni 1.5 zimetumika kununua mitambo miwilli aina ya Ozcan Kardesler Tip Cihazlari San,mitungi ipatayo 560 ya hewa tiba,gari la kusambazia mitungi ya Oksijeni pamoja na ujenzi wa jengo ambalo mitambo imefungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live